Rais Samia ahubiri 4R katika kuulinda na kuuendeleza Muungano

0
42

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Watanzania kuendeleza Muungano kwa kutekeleza falsafa ya maridhiano, kustahimiliana, kuleta mageuzi na kujenga nchi, kwani yataimarisha amani na utulivu wa kudumu pamoja na kuleta maendeleo endelevu.

Ameyasema hayo katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ambapo amesema kupitia Muungano, Tanzania imejenga umoja na mshikamano wa kitaifa kwa kuimarisha udugu, kupiga hatua kubwa ya maendeleo ya uchumi, siasa, kijamii pamoja na kudumisha mila na desturi.

“Nataka niwaambie Watanzania kwamba tuna kila sababu ya kujivunia muungano. Nchi hii Tanzania imetokana na maamuzi yetu wenyewe. Katika kipindi chote cha miaka 60 taifa hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania likiwa na watu wa makabila zaidi ya 120 wenye imani tofauti za kidini, kwa bahati njema tunaunganishwa na lugha moja ya taifa Kiswahili, tumeweza kuitunza na kuilinda nchi yetu kwa kudumisha amani na utulivu,” amesema Rais Samia.

Rais aelekeza vitabu vinavyoeleza mapito ya Muungano kutolewa kama zawadi

Aidha, Rais Samia ametoa wito kwa Watanzania kufanya kazi kwa bidii na kutumia maarifa zaidi ili kukuza tija kwa ustawi wa Taifa, kwani kazi ndio kipimo cha utu.

Kwa upande wake Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi katika hotuba yake, amesema kupitia muungano, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kuheshimika kimataifa huku ikiwa nchi ya mfano kwa wengine kutokana na kuwa na amani, umoja pamoja na mshikamano.

Send this to a friend