in ,

Rais aelekeza vitabu vinavyoeleza mapito ya Muungano kutolewa kama zawadi

Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza viongozi pamoja na Watanzania kwa ujumla kugawa vitabu vinavyoeleza mapito ya Muungano wa Tanzania kama zawadi kwa viongozi na wageni wa nchi za nje.

Ametoa kauli hiyo wakati akizindua vitabu vya Miaka 60 ya Historia ya Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na Kitabu cha Safari za Picha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 60 kwenye hafla iliyofanyika Ikulu, Chamwino ikiwa ni sehemu ya shamrashamra ya sherehe za Muungano ambapo pia amewatunuku Nishani viongozi mbalimbali waliopo madarakani pamoja na wastaafu.

Rais Samia amesema vitabu hivyo ni kumbukumbu muhimu kwa taifa na kwa Watanzania kwa kuwa watasoma na kupata taarifa mbalimbali ambazo hazipatikani kirahisi sehemu nyingine.

Aidha, amesema vitabu hivyo vitawawezesha kukuza ujuzi na kujiongezea maarifa kuhusu Muungano pamoja na kutunza historia inayoweza kutumika katika mambo kadhaa ikiwemo utalii.

Vile vile, Rais Samia amewasihi Watanzania kuendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano wa taifa kwa kufanya kazi kwa bidii na kudumisha uzalendo kwa kuuenzi kwa vitendo Muungano na waasisi wake.

Wanaodaiwa kusambaza picha za ngono WhatsApp wafikishwa mahakamani

Wanafamilia saba wakamatwa kwa kumchapa viboko ndugu aliyehudhuria maombi