TBS yasema vyakula vilivyotolewa na Marekani ni salama

0
38

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limesema msaada wa chakula uliotolewa na Wizara ya Kilimo ya Marekani kwa kushirikiana na Taasisi ya Jumuiya ya Kimataifa ulifuata taratibu za uingizwaji wa chakula nchini kwa kufanyiwa uchunguzi  na ukaguzi wa kimaabara.

Taarifa hiyo ni kufuatia taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na mchele ulioongezwa virutubishi, mafuta ya kupikia ya alizeti yaliyoongezwa virutubishi na maharage, vilivyotolewa katika baadhi ya shule za mkoa wa Dodoma chini ya mpango uitwao “Pamoja Tuwalishe.”

“TBS inapenda kuujulisha umma kuwa chakula hicho kilifuata taratibu za uingizwaji wa chakula nchini ambapo kilipofika kilifanyiwa ukaguzi na uchunguzi wa kimaabara na kilithibitishwa kuwa ni salama kwa matumizi. Aidha, utaratibu wa kuongeza virutubishi kwenye chakula unakubalika kitaalamu na hufanyika kwa lengo la kuboresha hali ya lishe kwa walaji,” imeeleza TBS.

DRC yaishtaki Rwanda Mahakama ya Afrika Mashariki

Aidha, TBS imesema itaendelea kusimamia kikamilifu jukumu la kuhakikisha kuwa chakula kinachoingia nchini kinakidhi vigezo vya usalama na ubora kwa mujibu wa matakwa ya viwango ili kuendelea kulinda afya za walaji.

Kwa upande wake Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ameitaka taasisi inayotekeleza mradi huo, iwaambie Marekani kuwa Tanzania kuna mchele na maharage, hivyo fedha wanazowapa wakulima wa Marekani wawape wakulima wa Tanzania na virutubisho viongezwe hapa nchini wakati Watanzania wakiwa wanaona.

Send this to a friend