in ,

DRC yaishtaki Rwanda Mahakama ya Afrika Mashariki

Mgogoro katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umechukua mkondo wa kisheria baada ya Kinshasa kuishtaki Rwanda katika Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ) jijini Arusha.

Kinshasa inadai kuwa Kigali imekiuka uhuru wa ardhi ya DRC na inaituhumu kwa kusaidia vita katika eneo hilo.

Katika maombi yake, DRC imeomba Rwanda kuzuiliwa kukiuka ardhi yake na kuondoa wanajeshi wake kutoka katika eneo ambalo inadai kuwa ni lao. Pia, DRC inataka mahakama itoe tamko kwamba vitendo vya Rwanda vimekiuka Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuhusu uadilifu wa ardhi.

“Katika kipindi cha miaka 25 iliyopita, Rwanda mara kadhaa imekiuka uhuru wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, uadilifu wa eneo lake la ardhi, na uhuru wake wa kisiasa,” sehemu ya maombi inasema.

Mbali na hilo, DRC inailaumu Rwanda kwa kutoa msaada kwa kundi la waasi la M23, ambalo linatuhumiwa kwa uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu ikidai kuwa msaada huo unakiuka pia mkataba wa EAC.

Kesi hii inajiri baada ya miaka mingi ya migogoro na jitihada za kidiplomasia kumaliza mzozo huo, ikiwa ni pamoja na juhudi za Mkutano wa Kimataifa wa Maziwa Makuu na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Fahamu chanzo cha kwikwi na namna ya kuizuia

Mabeyo: Hayati Magufuli alitaka kurudishwa nyumbani kabla ya kufariki