Wafanyabiashara wa mafuta Kenya hali tete baada ya Uganda kuichagua Bandari ya Tanga

0
87

Wafanyabiashara wa mafuta nchini Kenya wako katika hali mbaya baada ya Uganda kusisitiza msimamo wake wa kuanza mazungumzo na Tanzania ili kuagiza mafuta yake kupitia Bandari ya Tanga badala ya Bandari ya Mombasa kufuatia mzozo na Nairobi.

Awali, Uganda ilitangaza kuwa iko kwenye mazungumzo na Tanzania kutumia Bandari ya Dar es Salaam kuagiza mafuta yake baada ya Kenya kukataa kuipa kibali cha kutumia bomba lake.

Hata hivyo, umbali wa barabara kati ya Dar es Salaam na Kampala ni kilomita 1,715.6, ambayo ni urefu wa asilimia 49.5 zaidi ya umbali wa kilomita 1,147.6 kati ya Mombasa na Kampala.

Umbali huo mfupi unamaanisha kuwa Uganda inaokoa hadi $35 [TZS 89,250] kwa kila mita ya ujazo kwa kutumia Mombasa badala ya Dar es Salaam.

Wiki iliyopita iliibuka kuwa Uganda na Tanzania ziko katika mazungumzo ambayo yatashuhudia mafuta yaliyokuwa yakiingizwa nchini kupitia Bandari ya Tanga, ambayo ni karibu zaidi na Kampala.

Hata hivyo, chanzo cha mzozo kati ya Kenya na Uganda kinatokana na uamuzi wa Kampala mwaka jana wa kutangaza Kampuni ya Mafuta ya Taifa ya Uganda (UNOC) kama mwagizaji wa mafuta yote kwa ajili ya usambazaji kwa wafanyabiashara binafsi wa mafuta.

Serikali yatangaza kuwasajili madalali wa mazao

UNOC baadaye iliwasilisha maombi kwa Mamlaka ya Nishati na Mafuta ya Kenya (EPRA) Septemba 2023 ili kusajiliwa kama OMC nchini Kenya, ambayo ingeiwezesha kuagiza na kuuza mafuta kama OMC nyingine na kutumia bomba la Kenya Pipeline Company (KPC).

EPRA ilikataa maombi ya UNOC kwa sababu UNOC hakuweza kuthibitisha kiasi kinachohitajika cha mauzo ya kila mwaka ya lita milioni 6.6 ya petroli super, diesel (Automotive Gasoil), na/au kerosini (Jet A1) nchini Kenya.

Tangu wakati huo, Uganda imeishtaki Kenya katika Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ).

Send this to a friend