in , ,

Serikali yatangaza kuwasajili madalali wa mazao

Serikali imesema imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kwa ajili kudhibiti wafanyabiashara wanaoenda kinyume na bei elekezi ikiwa ni pamoja na kuendesha operesheni ya kuwakamata wafanyabiashara wanaoongeza bei kiholela.

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema Serikali imeanza utekelezaji wa sheria ya mwaka 2019 ya kuazisha Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) ambayo moja ya majukumu yake ni kudhibiti mazao yasiyokuwa na bodi.

“Pamoja na shughuli zake nyingine, mojawapo ni kuangalia mfumo unaoshughulika sokoni wa bei, mfumo wa masoko. Sasa hivi tunaanza kusajili madalali kwa sababu mazao yakitoka mkoani yakiingia Dar es Salaam, mtu wa kwanza anayepokea ni dalali, dalali ndiye anaye-determine [amua] soko kwa hiyo mkulima anaweza kupigwa na mlaji vilevile,” amesema.

Akizungumza kuhusu hali ya sukari nchini, Waziri Bashe amesema Serikali itaendelea kuagiza sukari nje ya nchi kwa mwaka huu zaidi ya tani laki tatu kutokana na hali mbaya ya uharibifu wa mashamba ya sukari uliotokana na mvua za El Nnino.

Kamati ya Bunge: Serikali idhibiti wavamizi wa mgodi wa Barrick Gold North Mara

Bashungwa aagiza mkandarasi aondolewe kwa kukosa vigezo