Watanzania 900 wapata kazi nchini Saudi Arabia

0
41

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Ali Mwadini amesema zaidi ya Watanzania 900 mwaka huu wamepata fursa ya kwenda kufanya kazi nchini humo kupitia utaratibu rasmi wa ajira.

Hayo yamebainishwa hapo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari wa Tanzania kwenye mkutano ulioendeshwa kwa njia ya mtandao ukilenga fursa mbalimbali zilizoko nchini humo.

“Hivi juzi kampuni kubwa ya Saudi Arabia ya Almarai ilikuja Tanzania kufanya interview [usaili] wa nafasi za kazi kwa Watanzania, walishirikiana na kampuni ya Mtemvu ambaye ni Mtanzania. Walipata Watanzania zaidi ya 500 kutoka Bara na wengine zaidi ya 400 kutoka Zanzibar waliochaguliwa kufanya kazi Saudi Arabia, hivyo fursa za ajira zipo,” amesema.

Utafiti: Sababu ya wagombea wa upinzani kutochaguliwa nchini

Aidha, amesema mbali na ajira hizo 900 mpya, kuna Watanzania 1,200 wanaofanya kazi Saudia kwa sasa na wanafanya kazi kwa mikataba rasmi inayotambulika na Serikali.

Mbali na hayo Balozi Mwadini amewasihi vijana wa Kitanzania kuchangamkia fursa za elimu zinazotolewa ambazo kwa mwaka Wizara ya Elimu nchini humo hutenga nafasi 160 za fursa ya masomo kwa ajili ya Watanzania, lakini vijana hawazichangamkii fursa hizo.

Send this to a friend