in , , ,

Utafiti: Sababu ya wagombea wa upinzani kutochaguliwa nchini

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti REPOA umeonesha kuwa Watanzania wana hofu ya kukosa huduma muhimu za kijamii endapo watamchagua kiongozi yeyote kutoka vyama vya upinzani hapa nchini.

Utafiti huo uliofanywa kwa kushirikiana na Taasisi ya Friedrich Ebert Stiftung kutoka nchini Ujerumani, ulihusisha watu 2,014 katika Wilaya za Ilala, Temeke, Ubungo, Kigamboni na Kinondoni mkoani Dar es Salaam, Karatu mkoani Arusha na Makete mkoani Njombe mwaka 2021.

Watumishi wanne wafukuzwa kazi kwa ubadhirifu wa fedha

Akiwasilisha utafiti huo, Mtafiti Mwandamizi wa REPOA, Dkt. Hubert Shija amesema kuna utaratibu kidemokrasia wa kuwa na vyama vingi unaosababisha wananchi kulalia chama kimoja.

“Utararibu wa kuchagua viongozi wa kisiasa katika Serikali za mitaa, Serikali kuu, Rais, wabunge na madiwani, tuliowahoji wanaona kwamba ukiipigia chama tawala ndiyo utapata huduma zaidi, ukiipigia chama cha upinzani unaweza usipate huduma zaidi kwa maana ya eneo na mgombea unayemchagua,” amesema.

Chanzo: Mwananchi.

Watumishi wanne wafukuzwa kazi kwa ubadhirifu wa fedha

Wanafunzi zao la elimumsingi bila ada kujengewa madarasa 8,000 kidato cha kwanza