Watumishi wa afya wapigwa marufuku kuchati kazini

0
63

Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Tumaini Nagu amewapiga marufuku watumishi wa afya katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini kuchati wakiwa eneo la kazi kwa kuwa wanashindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo.

Agizo hilo limefuata baada ya ongezeko la malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu ubovu wa huduma katika vituo vya afya, ambapo watumishi wa afya wamekuwa wakitumia muda mwingi kuchati kazini na kufanya mawasiliano binafsi kupitia simu zao za mkononi na kushindwa kuzingatia majukumu yao.

“Ni marufuku kuchati tukiwa kazini. Naomba nichukue nafasi hii kuwaambia watumishi wote wa sekta ya afya, ni marufuku kuchati kwa sababu tunapokuwa kwenye zamu chochote kinaweza kutokea. Mgonjwa anapokuwa hospitali yuko kwa ajili ya uangalizi,” amesema.

Wagoma kujiunga kidato cha kwanza kutokana na wahitimu kukosa ajira

Aidha, amewataka watumishi wa afya kuwa na lugha nzuri kwa wagonjwa na kuacha kuwapuuza na kutoa maneno yasiyopendeza pindi wanapotoa matatizo yao badala yake kuwa na upendo na kupenda kazi zao.

Kupitia agizo hilo, Mganga Mkuu wa Serikali amejitolea kuhakikisha kuwa huduma za afya zinaboreshwa na kwamba wananchi wanapata huduma bora na za haraka wanapohitaji matibabu katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Send this to a friend