in , ,

Tanzania kujiunga na mpango wa kusambaza chanjo wa COVAX

Tanzania inatarajia kujiunga na mpango wa kugawa chanjo ya Corona wa COVAX, Shirika la Afya Duniani limeeleza ambapo chanjo hizo zinaweza kuwasili nchini ndani ya wiki chache zaijazo.

“Tumepokea taarifa kuwa Tanzania sasa ipo katika mchakato wa kutaka kujiunga ja COVAX,” Mkurugenzi wa WHO wa afrika, Matshidiso Moeti amewaambia waandishi wa habari.

WHO imeeleza kuwa tayari Tanzania imechukua hatua za awali za kutuma maombi ya chanjo ya na kwamba sasa inaendelea na mpango mkakati wa namna ya kutoa chanjo kwa wananchi.

Richard Migigo wa Progaramu ya Maendeleo ya Kinga na Chanjo kwa Afrika ya WHO amesema kuwa wanatarajia kuwa chanjo hizo zitawasili nchini wiki kadhaa zijazo.

Tanzania ni miongoni mwa nchi chache za Afrika ambazo hazijaanza kutoa chanjo kwa raia wake.

Hivi karibuni Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) iliitaka Tanzania kutoa takwimu za maambukizi ya COVID19, sharti ambalo lililotaka na Tanzania kuomba $571 milioni kwa ajili ya kukabiliana na athari za ugonjwa huo kwenye uchumi.

Mara ya mwisho Tanzania ilitangaza takwimu hizo Mei 2020.

Hatua ya kuingiza chanjo nchini ni mwendelezo wa mkakati wa Rais Samia Suluhu Hassan wa kupambana na ugonjwa huo ambapo karibuni alisema kuwa Tanzania haiwezi kujitenga kama kisiwa.

Aliunda kamati ya kumshauri kuhusu namna ya kukabiliana na ugonjwa huo, na hivi karibuni iliwasilisha mapendekezo yake kwa Rais, na miongoni mwayo ni kutoa chanjo kwa wananchi hasa waliopo mstari wa mbele kupambana.

Siku 360 za Msulwa kwenye ukuu wa wilaya Morogoro

Rais Samia amlilia Mzee Kaunda