in ,

Siku 360 za Msulwa kwenye ukuu wa wilaya Morogoro

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Juni 15, 2021 ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba kwa kushindwa kusimamia Wafanyabishara wadogo (machinga).

Rais Samia ametangaza hatua hiyo wakati akihutubia vijana wa mkoa wa Mwanza na mikoa jirani waliowawakilisha vijana wote nchini.

Amesema amesikitishwa na kitendo cha Asakri Mgambo katika eneo la Kituo cha Mabasi Morogoro kuwanyanyasa Wafanyabishara wadogo maarufu kama wamachinga wanaofanya baishara nje ya Kituo hicho.

Rais amesema kitendo cha kunyanyaswa wafanyabishara hao si cha kiungwana na hakikubali kamwe.

Msulwa aliteuliwa kushika wadhifa huo Juni 21, 2020 akichukua nafasi ya Regina Chonjo ambaye alistaafu.

Kabla ya uteuzi huo Msulwa alikuwa Afisa Mwandamizi na Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Rais aiagiza BoT kujiandaa na matumizi ya sarafu za kimtandao (cryptocurrency)

Tanzania kujiunga na mpango wa kusambaza chanjo wa COVAX