in , ,

Taarifa ya serikali kuhusu ajira 260 za wahandisi

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa amesema katika kukabiliana na upungufu wa wahandisi nchini, ofisi yake imetoa kibali cha ajira 260 kwa ajili ya kujaza nafasi wazi katika Mamlaka za Serikali za mitaa.

Kwa upande wa watendaji wa kata, mtaa na vijiji amesema tathmini ya mahitaji halisi imeshafanyika na michakato ya kuandaa ajira hizo unaendelea.

Pamoja na mambo mengine alitumia nafasi hiyo kuwaelekeza waajiri kuendelea kushughulikia watumishi wenye vigezo na sifa za kupandishwa cheo kwa kuwatengea bajeti katika mwaka wa fedha ujao na kujiridhisha kuwa watumishi wote wanaostahili kutengewa bajeti ya kupandishwa vyeo wanatengewa nafasi.

“Waajiri wote nchini, wanapaswa kushughulikia madai ya watumishi na malimbikizo ya mishahara, hakikisheni mnaingiza madai ya malimbikizo ya mishahara katika mfumo wa HCMIS kama ilivyoelekezwa katika waraka wa utumishi wa umma,” ameelekeza.

Pia amewataka waajiri wote kuwasilisha orodha  za watumishi wenye sifa za kukaimu ili Ofisi hiyo iweze kukamilisha mchakato wa kujaza nafasi wazi za idara na vitengo.

“Hapa napenda kusisitiza kuwa waajiri waepuke kufanya upendeleo na unyanyasaji kwa watumishi kwa kuwakandamiza na kuwafanya washindwe kutekeleza majukumu yao kwa amani,” ameongeza.

Dereva Bodaboda arejesha milioni 115 alizookota

Mambo yanayosababisha saratani ya matiti na namna ya kujikinga