in ,

Mambo yanayosababisha saratani ya matiti na namna ya kujikinga

Mwezi wa Uhamasishaji wa Saratani ya Matiti, unaadhimishwa kote ulimwenguni ifikapo kila Oktoba, maadhimisho hayo hulenga kusaidia kuongeza umakini na msaada wa elimu kwa wanawake, ugunduzi wa mapema na pia huimarisha upatikanaji wa matibabu wa mapema wa ugonjwa huu baada ya kugundulika mapema.

SARATANI YA MATITI NI NINI?

Ni mabadiliko ya chembechembe hai zilizopo kwenye matiti. Saratani hii kwa kawaida haina dalili katika hatua za mwanzo. Wanawake katika hatua za mwanzo za ugonjwa hawana maumivu au dalili nyingine zozote.

Uchunguzi wa awali ndio utakaowezesha kuugundua ugonjwa, katika hatua hii mabadiliko yaletwayo na saratani ya matiti.

•  Kivimbe katika titi au kwenye makwapa.

• Mabadiliko ya umbo na ukubwa wa titi.

• Kutokwa na majimaji au damu katika chuchu ama chuchu kuingia ndani ya ziwa.

• Mabadiliko katika rangi ya ngozi ya titi (kuonekana kama sehemu ya nje ya ganda la chungwa).

MAMBO YANAYOCHANGIA KUPATA SARATANI YA MATITI

• Jinsi ya kike

• Kuanza hedhi katika umri mdogo.

• Kukoma siku katika umri mkubwa

• Kutozaa kabisa.

• Kutonyonyesha kabisa au kunyonyesha kwa muda mfupi.

• Utumiaji mafuta mengi katika chakula.

• Kutokufanya mazoezi ya mara kwa mara.

• Unene kupita kiasi

• Uvutaji sigara.

• Utumiaji wa pombe kupita kiasi.

• Historia ya saratani ya matiti katika familia.

JINSI YAKUJILINDA NA SARATANI YA MATITI

• Kujichunguza mwenyewe mara kwa mara kwa mara.

• Uchunguzi wa kitabibu wa matiti kila mwaka.

• Uchunguzi wa matiti kwa njia ya mashine ya mionzi (mara moja kwa mwaka kwa wenye miaka zaidi ya 40).

• Wanawake wote wenye umri kuanzia miaka 21 wajichunguze matiti yao siku ya 5-7 baada ya kumaliza hedhi mbele ya kioo.

HATUA  5 RAHISI ZA KUJICHUNGUZA MATITI

• Jiangalie katika kioo ukiwa umesimama wima na umeweka mikono kiunoni.

• Angalia kama kuna mabadiliko katika umbo au rangi ya ngozi ya titi na kama

           AU

• Ukiwa umesimama au umelala chali tumia mkono pamoja na kipaji cha vidole vya mkono wa kulia kuchunguza titi la kushoto na mkono wa kushoto kuchunguza titi la kulia kwa njia ya mzunguko.

• Kwa upole kamua chuchu ya kila titi na chunguza kama kuna ute ulio changanyika na damu.

• Muone daktari kama kuna uvimbe au ute ulio changanyika na damu au hali yoyote ulioiona wakati wa kujichunguza.

Taarifa ya serikali kuhusu ajira 260 za wahandisi

Historia: Simulizi fupi ya Brigedia Nyirenda walivyopandisha Mwenge wa Uhuru Mlima Kilimanjaro 1961