in ,

Polisi wafuta kesi 1,840 kwa kukosa ushahidi

Rais Samia Suluhu Hassan amemuagiza Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Ramadhan Kingai kuhakikisha unafanyika upelelezi ikiwa ni pamoja na kuwa na ushahidi wa kutosha kabla ya kumuweka mtuhumiwa mahabusu.

Amezungumza hayo leo Agosti 30 katika ufunguzi wa Kikao Kazi cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, Makamanda wa Polisi wa Mikoa na vikosi katika Shule ya Polisi Tanzania, wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.

Askari wasio na sifa ndio wanaolipa fedheha Jeshi la Polisi

Rais Samia amesema amepokea taarifa ya kesi 1,840 zilizofutwa kwa kutokuwa na ushahidi, ambapo baadhi ya Maafisa wa Polisi wamekuwa wakitumia nafasi zao kuwabambikizia kesi raia wasiokuwa na hatia kwa maslahi yao binafsi.

“Kikao kilichopita nilitoa maagizo, kabla hujampeleka mtu ndani hakikisha umefanya kazi yako vizuri, una ushahidi wa kutosha ndipo unakwenda kumsweka [kumpeleka mahabusu] lakini umemkamata hujapeleleza umeambiwa tu huyo msweke huko ndani, huo ni mzigo kwa Serikali na mzigo kwa familia,” amesema Rais Samia.

Rais Samia: Askari wasio na sifa ndio wanaolipa fedheha Jeshi la Polisi

Marufuku ulaji nyama ya nguruwe