in ,

Tanzania kuunga mkono hatua za kurejesha amani Somalia

Rais Samia Suluhu Hassan amesema katika mazungumzo yake na Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia, Dkt. Hassan Sheikh Mohamud, amewahakikishia Tanzania kuendelea kuunga mkono jitihada za kurejesha amani na iko tayari kutoa mafunzo katika nyanja mbalimbali.

Ameyasema hayo leo wakati yeye na Rais wa Somalia aliyepo nchini Tanzania kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili wakizungumza na vyombo vya habari katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu, jijini Dar es Salaam.

“Kama mnavyojua hali ya wenzetu [Somalia] haiko vizuri sana, kwahiyo tumewahakikishia kuwaunga mkono kwenye kujenga uwezo wa wao kama nchi kujilinda wenyewe,” amesema.

Rais Samia ahubiri 4R katika kuulinda na kuendeleza muungano

Aidha, amesema licha ya Tanzania na Somalia kuwa na mwingiliano kwa miaka mingi, ziara hiyo imetoa fursa ya kujadili na kuona umuhimu wa kuwa na mfumo rasmi wa kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili.

Pamoja na hayo, amesema viongozi wa Afrika hawana budi kudumisha umoja kama walivyodhamiria waasisi wa Umoja wa Afrika ili kuikaribia azma ya kujenga mtangamano.

Makonda aagiza barabara itengwe kwa ajili ya maonesho ya biashara kwa wajasiriamali

Wafikishwa mahakamani kwa kuwahadaa wanaume kimapenzi na kuwaibia