in ,

Tanzania na China kuanzisha mfumo wa upatikanaji wa vifaa tiba vya matibabu ya moyo

Nchi za Tanzania na China zimekubaliana kuanzisha mfumo wa wa pamoja wa upatikanaji wa vifaa tiba vinavyotumika kutoa huduma za matibabu ya moyo kutoka nchini China kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo na kutarajiwa kurahisisha upatikanaji wa vifaa vinavyotumika kutoa huduma za matibabu ya moyo na matibabu mengine yanayohitaji vifaa tiba.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya Naibu Waziri Mkuu kutoka Serikali ya watu wa China, Liu Guozhong ambapo Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema katika majadiliano na Naibu waziri huyo, China imekubali kutoa msaada wa vifaa tiba nchini pamoja na kuanza kwa ushirikiano wa kuagiza vifaa tiba nchini China.

“Tumekubaliana kupitia Bohari ya Dawa (MSD) tutaenda kushirikiana na Serikali ya Watu wa China kupata vifaa tiba ambavyo mara nyingi tumekuwa tukiviagiza katika mataifa ya mbali na kuchukua muda mrefu kutufikia,” amesema.

Mikoa 5 inayoongoza kwa ndoa za utotoni Tanzania

Dkt. Mollel amesema Tanzania imejipanga kuhakikisha kuwa Bohari ya Dawa (MSD) inaenda moja kwa moja katika viwanda vilivyopo nchini China kununua vifaa tiba hivyo ili kupunguza gharama za matibabu.

“Tanzania tayari tuna sayansi kubwa, lakini vifaa mbalimbali vinavyotumika kila siku katika kutoa huduma za matibabu havipatikani hapa nchini kwasababu hatuna viwanda vinavyozalisha vifaa hivyo,” ameongeza.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge amesema JKCI imekuwa moja ya Taasisi kubwa zinazotoa huduma za matibabu ya mogonjwa ya moyo barani Afrika, na kuwa yakwanza kufanya.

Rais Samia: Vijana wanatoroka kujiunga na vikundi vya ugaidi nje ya nchi

Jinsi ya kujua ikiwa ‘link’ ya barua pepe si salama