in , , ,

Jinsi ya kujua ikiwa ‘link’ ya barua pepe si salama

Ulaghai kupitia barua pepe, unaojulikana kama ‘phishing,’ ni aina ya udanganyifu mtandaoni ambao wadukuzi hutumia kwa lengo la kupata taarifa binafsi kutoka kwa watu, kama vile majina, nywila, na habari za kifedha. Hapa kuna maelezo zaidi kuhusu jinsi ulaghai huo unavyofanya kazi.

Hapa kuna njia rahisi na zenye ufanisi za kuchunguza ikiwa ‘link’ ya barua pepe ni salama kubofya. Vidokezo hivi vitakusaidia kuepuka kubonyeza viungo vinavyoweza kukupeleka kwenye tovuti za ulaghai.

Kagua ‘link’
Mojawapo ya njia bora ya kujua ikiwa link ni salama ni kuichunguza kabla ya kubofya. Unaweza kusogeza kwa uangalifu mausi yako juu ya link na kutazama anwani ya wavuti inayoonekana. Ikiwa anwani ya wavuti inaonekana kutiliwa shaka, imeandikwa vibaya, au haijulikani, usibofye.

Angalia barua pepe kwa makini
Wasiliana na mtumaji wa barua pepe moja kwa moja kama una mashaka. Ikiwa barua pepe inadai kutoka kwa shirika fulani, tembelea tovuti yao rasmi au tumia mawasiliano yao ya moja kwa moja kuthibitisha uhalali wa barua pepe.

Tumia huduma ya kupima ‘links’
Kuna huduma mtandaoni zinazoruhusu watumiaji kuchunguza ‘links’ kwa usalama. Unaweza kutumia huduma kama vile “Link Scanner” au “URL Unwinding” ili kuchambua link na kutoa habari zaidi juu ya usalama wake. Hata hivyo, kuwa mwangalifu na kutumia huduma hizo kutoka kwa vyanzo vya kuaminika.

Nenda moja kwa moja kwenye tovuti ya kampuni
Ukiwa na shaka, nenda moja kwa moja kwenye tovuti ya kampuni kwa kuandika mwenyewe anwani ya tovuti, au kutafuta tovuti katika mtambo wa kutafuta. Mara nyingi, matokeo ya kwanza au ya pili yanayokuja ni halali. Ukiona neno ‘sponsored’ juu ya matokeo ya utafutaji, chukua muda kabla ya kubonyeza na fikiria kubonyeza matokeo ya chini yake.

Hakiki mpokeaji wa barua pepe
Hakikisha barua pepe inatoka kwa chanzo halali na sio bandia au feki. Wahalifu mara nyingine hutumia tofauti ndogo au kujifanya kuwa vyanzo halali. Unaweza kufanya hivyo kwa kutazama anwani ya barua pepe na jina la mpokeaji. Ikiwa anwani ya barua pepe au jina halifanani na utambulisho wa mpokeaji, usiamini barua pepe hiyo.

Jiulize maswali matatu kabla hujabonyeza ‘link’
Unapokaribia kubonyeza, jipe muda. Kabla ya kubonyeza kiungo ‘link’ au ‘attachment’ yoyote ya barua pepe, chukua muda wa kuvichunguza na kujiuliza maswali haya matatu;

Je! Ninamfahamu mtumaji?
Je! Nawatilia shaka?
Je! Nilitarajia kutoka kwao kuniletea ‘link’ au kiambatisho (attachment)?

Ikiwa jibu ni hapana kwa mojawapo ya maswali haya, basi usibonyeze kiungo chochote au kufungua. ‘Links’ au ‘attachment’ za barua pepe zinaweza kuonekana kuwa visizo na madhara, lakini wanaweza kujumuisha programu hasidi inayoweza kuharibu kifaa chako au kuiba data yako. Ni bora kuwa na tahadhari kuliko kujuta linapokuja suala la viambatanisho vya barua pepe.

Tanzania na China kuanzisha mfumo wa upatikanaji wa vifaa tiba vya matibabu ya moyo

Polisi waruhusu maandamano ya CHADEMA