in , ,

Corona: TBS yataja mambo 7 ya kuzingatia kwa wazalishaji na watumiaji wa barakoa za vitambaa

Katika kuhakikisha wananchi wanakuwa salama wanapotumia vifaa kinga mbalimbali kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetoa matakwa ya kuzingatiwa wakati wa uzalishaji na utumiaji wa barakoa za kitambaa (cloth face mask).

Shirika hilo limesema matakwa ya msingi ambayo yanapaswa kuzingatiwa na wazalishaji, wasambazaji na watumiaji wa barakoa hizo ni;

  1. Kitambaa kiwe cha pamba (cotton) kwa asilimia 100
  2. Kitambaa kiwe na uzito wa GSM 90-130
  3. Barakoa iwe na tabaka (layers) zisizopungua mbili
  4. Barakoa iwe na uwezo wa kuruhusu upumuaji kwa urahisi
  5. Iweze kuvalia na kufunika pua na mdomo vizuri
  6. Kitambaa kisiwe chenye kuchuja rangi (kwa kitambaa chenye rangi)
  7. Iweze kufuliwa na kunyooshwa kwa pasi au kuanikwa juani bila kuathiri ubora wa kitambaa

Aidha, shirika hilo limesema linaendelea na maandalizi ya viwango mbalimbali vya vifaa vya kinga binafsi (Personal Protective Equipments-PPE).

RC Gambo aeleza Kenya inavyotumia corona kuua utalii Tanzania

Spika Ndugai na Cecil Mwambe washtakiwa Mahakama Kuu ya Tanzania