in ,

Sabaya aagiza polisi kukamata wasiotoa/dai risiti

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ameiagiza kamati ya ulinzi na usalama kusaidiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwakamata wafanyabiashara na wateja wanaouza na kununua bidhaa bila kutoa na kudai risiti.

Sabaya ametoa agizo hilo wakati akizungumza na watendaji wa TRA, maafisa biashara wa halmashauri pamoja na watendaji wanaohusika na masuala ya fedha kuhusu kuongeza mapato ya wilaya hiyo katika mwaka wa fedha 2020/21.

Amesema wasiotoa au kudai risiti wamekuwa wakisababisha Serikali kukosa mapato stahiki na mamlaka hiyo kushindwa kufikia malengo ya ukusanyaji kodi na maduhuli ya serikali.

“Utakuta mtu ananunua mzigo wa mamilioni ya fedha hadai risiti au anafanyia ujanja ujanja wa kupata risiti iliyoambatana na biashara iliyofanyika, kamateni weka ndani tupate mapato tujenge barabara, shule, hospitali, tununue dawa na kuleta maendeleo kwa wananchi,” amesema

Ametumia nafasi hiyo kueleza kwamba hakuna duka wala akaunti ya mfanyabishara iliyofungwa na TRA bali wafanyabiashara wamekuwa wakitoa bidhaa nje ya maduka na kuwapa wafanyabiashara wadogo wakauze nje na baadaye hupeleka faida kupewa posho yake ya siku hivyo, jambo linalosababisha TRA kukosa mapato.

TRA wilayani Hai imesema inakusudia kukusanya kiasi TZS bilioni 4.6 kwa mwaka wa fedha wa 2020/21.

Apata faida TZS bilioni 6 kwa kuuza chanjo bandia ya Corona

Historia fupi ya Seif Sharif Hamad (1943-2021)