in ,

Tifu TV yafungiwa sakata la urushaji matangazo msiba wa Maalim Seif

Tume ya Utangazaji Zanzibar imeifungia kituo cha televisheni, Tifu TV, kwa siku saba kwa madai ya kukiuka mwongozo wa urushaji matangazo kipindi hiki cha msiba Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad.

Katibu Mtendaji wa tume hiyo, Omar Said amesema licha ya kutolewa mwongozo wa urushaji wa matangazo, kituo hicho hakikutii, na hivyo hatua hiyo imechukuliwa ili iwe fundisho kwa vituo vingine.

Mwongozo huo unavutaka vituo vya televisheni, redio, mitandao ya kijamii kurusha vipindi maalum vya maombolezo katika muda wa siku saba za maombolezo ya kifo cha nguli huyo wa siasa.

“Hatukutaka kuchukua maamuzi haya kwa chombo hiki, lakini kutokana na kukiuka maadili ya muongozo uliotolewa, imelazimika kuchukua uamuzi huo, ifahamike kwamba maamuzi haya yamekuja kufuatia majadiliano na vyombo vingine mbalimbali vya Serikali, juu ya kitendo hicho, na ikaamuliwa kwa pamoja kichukuliwe hatua za kinidhamu,” ameeleza kiongozi huyo.

Historia fupi ya Seif Sharif Hamad (1943-2021)

Taarifa ya TMA kuhusu kuanza mvua za masika