in ,

Mahakama yafuta kesi ya Wakili Madeleka kwa kushindwa kuiendesha

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha imeridhia kufuta maombi ya Wakili Peter Madeleka ya kufungua shauri dhidi ya Kamati ya Maadili ya Mawakili baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwasilisha maombi ya shauri la nidhamu mbele yake.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya mahakama na wajibu maombi kukubaliana kufutwa kwa maombi hayo kutokana na Wakili Madeleka kushindwa kuyaendesha licha ya mahakama kumpa nafasi mara kwa mara.

Wakili huyo alifungua maombi hayo Februari 26, mwaka huu kwa lengo la kuizuia Kamati hiyo kumuita mbele yake.

Mahakama imeeleza kuwa Wakili Madeleka alijaribu kuchelewesha kusikilizwa kesi hiyo kwa kuweka vipingamizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuweka pingamizi dhidi ya Wakili wa Serikali aliyeandaa kiapo, pamoja na kuizuia Mahakama kusikiliza shauri hilo akidai kuwa ameshafungua shauri la rufaa katika Mahakama ya Rufaa, na kumtaka Jaji Joachim Tiganga kujindoa kwani hana imani naye.

“Baada ya kupitia na kupima hoja za mleta maombi za kukataa kuendelea na shauri hilo, Jaji Tiganga alikataa kujiondoa na kumtaka mleta maombi alete hoja zake katika shauri la msingi ili asikilizwe na hatimae kutolewa maamuzi.

Watumishi wa bandari watakiwa kuchagua kati ya TPA au DP World

Hata hivyo, Wakili Madeleka aligomea maelekezo hayo, akasimama na kuondoka mahakamani. Kufuatia tabia hiyo ya utovu wa nidhamu aliyoinesha, Jaji Tiganga aliuliza upande wa wajibu maombi kama walikuwa na hoja yoyote, wajibu maombi wakaomba maombi hayo yafutwe kwa kuwa Wakili Madeleka ameshindwa kuyaendesha,” imesema taarifa ya Mahakama.

Taarifa imefafanua kuwa kabla ya mahakakama kufikia uamuzi huo, Wakili Madeleka alijinasibu kwa maandishi kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii kwamba alikuwa na nia ya kuchelewesha shauri hilo, kwani maandishi yake yanahusiana na shauri alilofungua mahakakamani.

Mahakama imesema baadhi ya maandishi ambayo aliambatisha na nakala ya pingamizi katika shauri hilo aliandika, “sikilizeni, yote yanayofanywa na Mahakama yanapaswa kuzingatia Ibara ya 107B ya Katiba ya Tanzania. Hapo nitaanza na pingamizi la kisheria.”

Andiko lingine likiwa “ Zile njama za kunifuta uwakili zinabidi zisubili kwanza mpaka mwaka 2047. Kamati ya Mawakili imeitwa mbele ya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha kwa tuhuma za utovu wa maadili” pamoja na maandiko mengine.

Nchi 10 za Afrika zenye idadi kubwa ya ndege mwaka 2024

Kampuni 30 zautaka mradi wa Mwendokasi